Aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa amechukua Fomu rasmi ya kugombea urais kupitia tiketi ya Chadema.
Lissu amesema uamuzi wa kumsimamisha mgombea huyo haukuwa wa kukurupuka bali umefuata uchunguzi wa muda usiopungua miezi mitatu na kujiridhisha kuwa Lowassa anafaa kuwa mgombea urais chini ya chama hicho.
Amesema katiba ya Tanzania inasema pamoja na mambo mengine mtu pakee anayezuiwa kugombea urais ni yule aliyekutwa na hatia na Mahakama ndani ya kipindi cha miaka mitano, hivyo Chadema imepekua Nyaraka zote za kimahakama nchini na kujiridhisha kwamba Lowassa hana hatia yoyote inayoweza kumzuia kugombea nafasi ya urais.
Source: BBC Swahili