
Mkazi wa Shikombe wilayani Geita, Buhula Ngassa (47) amekamatwa
na vitambulisho 43 vya wapiga kura, hata hivyo amedai vilikuwa vya
wateja wake waliofika kwake kusajili simu.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Geita, Joseph Konyo amesema leo kuwa mtuhumiwa Ngassa
alikutwa na vitambulisho vya zamani 7 na 36 ni vipya ambavyo
vitengenezwa kwa kutumia teknolojia ya BVR.
Kamanda
Konyo ameongeza mtuhumiwa amejitetea kuwa vitambulisho hivyo vilikuwa ni
kwa ajili ya kuwasajilia wateja waliofika kwake...