Tangaza Biashara yako na Hundred Radio

Fikia maelfu ya watu kwa kutangaza biashara yako nasi hapa, wasiliana nasi ili kuweza kutangaza nasi. Karibuni wote

Hundred Radio Online

The best Online Radio in Tanzania and all over the World. Keep Listening everyday.

Pata Modem za Vodacom

Pata Modem za Vodacom kwa Tsh 25,000/= tu na upate kifurushi cha 5GB

Fly Safe with Fast Jet

For affordable price Fly with fast Jet in various regions in Tanzania.

Be A Sponsor

Contact us if u want to be one of our sponsors.

Monday, August 10, 2015

Maelfu wamsindikiza Lowassa kuchukua fomu NEC


Aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa amechukua Fomu rasmi ya kugombea urais kupitia tiketi ya Chadema.

Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu amesema baada ya kuchukua fomu hizo Lowassa atakuwa tayari kuzunguka nchi nzima kujitambulisha kwa wananchi kama mgombea rasmi wa Chadema.
Lissu amesema uamuzi wa kumsimamisha mgombea huyo haukuwa wa kukurupuka bali umefuata uchunguzi wa muda usiopungua miezi mitatu na kujiridhisha kuwa Lowassa anafaa kuwa mgombea urais chini ya chama hicho.
Amesema katiba ya Tanzania inasema pamoja na mambo mengine mtu pakee anayezuiwa kugombea urais ni yule aliyekutwa na hatia na Mahakama ndani ya kipindi cha miaka mitano, hivyo Chadema imepekua Nyaraka zote za kimahakama nchini na kujiridhisha kwamba Lowassa hana hatia yoyote inayoweza kumzuia kugombea nafasi ya urais.

Source: BBC Swahili

Tuesday, July 28, 2015

Adakwa na vitambulisho zaidi ya 40 vya kura


Mkazi wa Shikombe wilayani Geita, Buhula Ngassa (47) amekamatwa na vitambulisho 43 vya wapiga kura, hata hivyo amedai vilikuwa vya wateja wake waliofika kwake kusajili simu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Joseph Konyo amesema leo kuwa mtuhumiwa Ngassa alikutwa na vitambulisho vya zamani 7 na 36 ni vipya ambavyo vitengenezwa kwa kutumia teknolojia ya BVR.
Kamanda Konyo ameongeza mtuhumiwa amejitetea kuwa vitambulisho hivyo vilikuwa ni kwa ajili ya kuwasajilia wateja waliofika kwake wakihitahitaji huduma hiyo hivyo alikuwa anaenda maeneo ya mjini ili avidurufu na kupata kumbukumbu atakazoziwasilisha kwa kampuni za simu.
Hata hivyo RPC Konyo amesema uchunguzi zaidi unaendelea kubaini ukweli wa sakata hilo. Awali, ilidaiwa kuwa mtuhumiwa alikamatwa na vitambulisho 200 vya kura lakini Jeshi la Polisi Geita limethibitisha kuwa ni 43 pekee.

Lowassa Ndani ya UKAWA


“Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje”. Hii ni moja ya kauli  ambayo Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliziongea Arusha May 30 2015 alipotangaza nia ya Kugombea Urais kupitia CCM.
 
CCM ilikuwa na Wagombea zaidi ya 40 ambao walitangaza nia na kuchukua fomu za Kugombea Urais 2015 lakini baadae Chama hicho kikampitisha Dk. John Pombe Magufuli kugombea nafasi hiyo, baada ya hapo kukawa na  taarifa nyingi sana kuhusu ishu ya Edward Lowassa na UKAWA.
 
Viongozi wa Umoja wa UKAWA wamekutana Dar  leo  na mmoja wa Viongozi hao, James Mbatia amesema wamekubaliana kumkaribisha Mbunge Edward Lowassa ndani ya UKAWA na wako tayari kumpa nafasi na kushirikiana nae.

Mbatia  ameongeza kuwa Lowassa ni mchapa kazi makini na mfuatiliaji wa karibu wa kiutendaji katika majukumu anayokabidhiwa.
 
Alipoulizwa kuwa Lowassa atakuwa mgombea Urais Mbatia amesema kila chama kina utaratibu wake  hivyo mchakato ukishakamilika  atatangazwa mgombea urais wa UKAWA mmoja  mwanzoni mwa mwezi agosti.

SIKILIZA HUNDRED RADIO ONLINE KILA SIKU
CLICK: www.mixlr.com/hundred-radio

Monday, July 13, 2015

Dk Magufuli Achaguliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kupitia chama hicho. Anandika Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Katika Mkutano Mkuu uliofanyika usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma, Dk. Magufuli amechaguliwa kwa kura 2104 sawa na asilimia 87.08, akifuatiwa na Balozi Amina Salum Ali aliyepata kura 253 sawa na asilimia 10.4 na Asha-Rose Migiro aliyepata kura 59 sawa na asilimia 2.44702.